Kuhusu Sisi

Historia Fupi

Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (ZCSRA) ni muungano wa Taasisi mbili zilizokuwa na mamlaka kamili za kiutendaji, ofisi zenyewe ni Ofisi ya Mrajisi wa Vizazi na Vifo na Ofisi ya Usajili na Kadi za Utambulisho Zanzibar. Ofisi hii imeanzishwa kwa Sheria Namba 3 ya 2018, ina majukumu ya kusajili Matukio ya kijamii na kutoa vyeti maalum, matukio hayo ni Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na Wasiokua Wazanzibari Wakaazi.

  •  Vizazi
  •  Ndoa
  •  Talaka
  •  Vifo
  •  Utambulisho

Kimuundo Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii inaongozwa na Bodi ya Ushauri ya Wakala chini ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo na Mkurugenzi Mtendaji ambaye ameteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

DHAMIRA ZA TAASISI

Kutoa kumbukumbu na takwimu muhimu zilizotokana na matumizi ya mifumo ya kisasa ya usajili wa matukio ya kijamii ili kuhakikisha kwamba Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii ni taasisi imara na inayoaminika

Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuchukua, kushughulikia, kuchambua, kutoa taarifa na kuhifadhi kumbukumbu za matukio ya kijamii

DIRA YA TAASISI

Kuwa ni mfano wa kuigwa katika usajili na utambuzi wa jamii katika kiwango ambacho kufikia mwaka 2030 hakutakua na mtu hata mmoja ambae hajatambuliwa na kurikodiwa

Malengo ya Taasisi

Usajili

Kufikia usajili kamili wa matukio ya kijamii

Uwezo na Utendaji

Kuimarisha uwezo wa utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii

Uwezo wa Kuhudumu

Kuimarisha uwezo wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii katika kutoa huduma

Kuboresha Mifumo

Kuanzisha Mifumo ya Usimamizi wa Taarifa

Kisheria

Kuimarisha mazingira ya kisheria ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii

Uhusiano na Wadau

Kuimarisha hali ya kuaminika kwa jamii na uhusiano na Wadau