Mzanzibari Mkaazi

Gharama


Muombaji asiezidi miaka 25:

Hakilipiwi (Bure)

Muombaji aliezidi miaka 25:

Bei : 20,000/= (Tzs)

Aliepoteza kwa mara ya kwanza/Kuharibika:

Bei : 20,000/= (Tzs)

Anaehitaji marekebisa kwa mara ya 2:

Bei : 30,000/= (Tzs)

Kubadilisha taarifa:

Bei : 20,000/= (Tzs)

Mzanzibar Mkaazi


Kifungu cha 27 kinazungumzia kuanzishwa kwa regista la Utambulisho kwa ajili ya usajili na utoaji wa kadi za Utambulisho.

Utaratibu:
  • Anatakiwa awe Mzanzibari kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari namba 5 ya 1985
  • Awe anaishi Zanzibar kwa makazi yake ya kudumu.
  • Awe ametimiza miaka 18 na kuendelea
  • Afike mwenyewe katika Afisi ya Wakala akiwa na barua ya sheha wa Shehia anayoishi na cheti cha kuzaliwa
  • Wakala inaweza kudai uthibitisho mwengine kwa kadri atakavyotoa taarifa kwa afisa wa Usajili
Utaratibu Nje Ya Wakati (Zaidi ya miaka 25):
  • Cheti cha kuzaliwa kilichohakikiwa
  • Awe na barua ya sheha
  • Barua Rasmi ya maombi binafsi ya kupatiwa Kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi
  • Taarifa ya mmoja kati ya taarifa za wazazi wake(Cheti au Kitambulisho)
  • Afike mwenyewe Afisi kuu ya Vitambulisho Mazizini kwa ajili ya mahojiano