Kuhusu Sisi

Historia Fupi

Wakala wa Usajili wa matukio ya Kijamii Zanzibar ni muungano wa Taasisi mbili zilizokuwa na mamlaka kamili za kiutendaji, ofisi zenyewe ni Afisi ya Vizazi na Vifo na Afisi ya Usajili na Kadi za Utambulisho Zanzibar. Afisi hii imeanzishwa kwa Sheria Namba 3 ya 2018, ina majukumu ya kusajili Matukio ya kijamii na kutoa vyeti maalum, matukio hayo ni Vizazi, Vifo, Ndoa, Talaka na Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi na wasiyokua Wazanzibari Wakaazi.

  •  Vizazi
  •  Ndoa
  •  Talaka
  •  Vifo
  •  Utambulisho

Afisi ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii inaongozwa na Bodi ya Ushauri chini ya Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mtendaji ambae ameteuliwa na Rais wa Zanzibar na Baraza la Mapinduzi

DHAMIRA ZA TAASISI

Kutoa kumbukumbu na takwimu muhimu zilizotokana na matumizi ya mifumo ya kisasa ya usajili wa matukio ya kijamii ili kuhakikisha kwamba Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii ni taasisi imara na inayoaminika

Kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuchukua, kushughulikia, kuchambua, kutoa taarifa na kuhifadhi kumbukumbu za matukio ya kijamii

DIRA YA TAASISI

Kuwa ni mfano wa kuigwa katika usajili na utambuzi wa jamii katika kiwango ambacho kufikia mwaka 2030 hakutakua na mtu hata mmoja ambae hajatambuliwa na kurikodiwa

Malengo ya Taasisi

Usajili

Kufikia usajili kamili wa matukio ya kijamii

Uwezo na Utendaji

Kuimarisha uwezo wa utendaji kazi wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii

Uwezo wa Kuhudumu

Kuimarisha uwezo wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii katika kutoa huduma

Kuboresha Mifumo

Kuanzisha Mifumo ya Usimamizi wa Taarifa

Kisheria

Kuimarisha mazingira ya kisheria ya Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii

Uhusiano na Wadau

Kuimarisha hali ya kuaminika kwa jamii na uhusiano na Wadau