Gharama
-
Muombaji asiezidi miaka 25:
Hakilipiwi (Bure)
-
Muombaji aliezidi miaka 25:
Bei : 20,000/= (Tzs)
-
Aliepoteza kwa mara ya kwanza/Kuharibika:
Bei : 20,000/= (Tzs)
-
Anaehitaji marekebisa kwa mara ya 2:
Bei : 30,000/= (Tzs)
-
Kubadilisha taarifa:
Bei : 20,000/= (Tzs)
Mzanzibar Mkaazi
Kifungu cha 27 kinazungumzia kuanzishwa kwa regista la Utambulisho kwa ajili ya usajili na utoaji wa kadi za Utambulisho.
Utaratibu:
- Anatakiwa awe Mzanzibari kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzibari namba 5 ya 1985
- Awe anaishi Zanzibar kwa makazi yake ya kudumu.
- Awe ametimiza miaka 18 na kuendelea
- Afike mwenyewe katika Afisi ya Wakala akiwa na barua ya sheha wa Shehia anayoishi na cheti cha kuzaliwa
- Wakala inaweza kudai uthibitisho mwengine kwa kadri atakavyotoa taarifa kwa afisa wa Usajili
Utaratibu Nje Ya Wakati (Zaidi ya miaka 25):
- Cheti cha kuzaliwa kilichohakikiwa
- Awe na barua ya sheha
- Barua Rasmi ya maombi binafsi ya kupatiwa Kitambulisho cha Mzanzibar Mkaazi
- Taarifa ya mmoja kati ya taarifa za wazazi wake(Cheti au Kitambulisho)
- Afike mwenyewe Afisi kuu ya Vitambulisho Mazizini kwa ajili ya mahojiano